Baraka FM

Viongozi wa dini watakiwa kutenda kazi bila upendeleo

22 October 2024, 07:29

Askofu Mkuu wa kanisa la Jehovah Nis Pentecost Church Tanzania(picha na Ezra Mwilwa)

Viongozi wa Dini wameazwa kulitumikia kanisa na watu mbalimbali bila kujali itikadi za kidini wala kabila.

Na Ezra Mwilwa

Wachungaji na viongozi wengineo wa makanisa wametakiwa kutenda kazi ya Mungu bila upendeleo wowote katika kuhudumia watu.
Wito huo umetolewa na Dr.Askofu Abihud Simkoko wakati akiwabariki wachungaji wa kanisa la Jehovah Nis Pentecost Church Tanzania Airport ya Zamani amesema watumishi wafanye kazi bila kubagua dini wala kabila.

Sauti ya Askofu Abihud Simkoko akiwabariki wachungaji

Nao baadhi ya ya wachungaji walio pata mbaraka huo wameahidi kulitumikia kanisa na watu wote kwa moyo wote.

Baadhi ya Wachungaji walio bata Mbaraka(picha na Ezra Mwilwa)
Sauti za wachungaji walio pata mbaraka

Katika hatua nyingine Askofu Simkoko amewaweka wakifu na kuwaingiza kazini viongozi wa Umoja wa wanawake katika kanisa hilo ngazi ya Taifa na kuwataka wawe na mshikamano.

Askofu Simkoko akiongea na Vingozi wa Umoja wa wanawake na wachungaji walio pata mbaraka (picha na Ezra Mwilwa)
Sauti ya Askofu Simkoko akiwasimika viongozi wa umoja wa wanawake

Nae mwenyekiti wa umoja wa wanawake kanisa ngazi ya Taifa Mchungaji Sophia Mwazembe amewaomba wanawake wenzake kuwa na umoja mshikamano kwa kuitenda kazi ya Mungu.

Sauti ya mwenyekiti wa umoja wa wanawake Mchungaji Sophia Mwazembe