Baraka FM

Kanisa la Moravian laleta tabasamu Mbarali kupitia 21 mission

21 October 2024, 18:53

Baadhi ya wananchi na viongozi wa kanisa la Moravian wakipokea maelezo kutoka kwa mratibu wa mradi wa Tree project ndani ya mission 21 Thobias Teobadia

Taasisi mbalimbali nchini zinawajibu wa kuisaidia jamii kuondoa changamoto ambazo zinaikabili katika nyanja mbalimbali.

Na Mch.Bosco Nyambege

Wananchi wa Kijiji Cha Luhanga kata ya Luhanga wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wamelishukuru Kanisa la Moravian Tanzania jimbo la kusini magharibi kupitia mradi wa mission 21 Kwa kuwatatulia tatizo la maji lililokuwa likiwakabili muda mrefu.

Wakizungumza na baraka FM wakati wa uzinduzi wa kisima kilichochimbwa na shirika Hilo, baadhi ya wananchi jamii ya kifugaji wamesema awali walikuwa wakitembea zaidi ya kilometa 20 kutafuta huduma ya maji lakin Kwa Sasa wamesogezewa huduma hiyo.

Wamesema kuanzishwa Kwa mradi huo katika jamii Yao pia itasaidia mifugo Yao kupata maji na kuepusha migogoro iliyokua ikijitokeza kipindi Cha nyuma baina Yao na wakulima.

Baadhi ya wananchi jamii ya wafugaji katika Mkutano wa uzinduzi wa mradi wa maji uliotekelezwa na kanisa la Moravian Jimbo la kusini magharibi kupitia mission
Sauti za baadhi ya wananchi jamii ya kifugaji

Awali akisoma risala Kwa mgeni rasmi Roida Tayai Satulo amesema mbali ya mradi huo kuwapatia maji pia shirika Hilo kupitia mradi wa Tree project imewawezesha kuazisha vitalu vya miti mbalimbali ambayo itasaidia kuondoa ukame unaolikumba eneo kubwa ndani ya Wilaya ya Mbarali.

Sauti ya msoma Risala risala Kwa mgeni Roida Tayai Satulo

Naye diwani wa kata hiyo Baraka Leteyo amelishukuru KMT- JKM kupitia mission 21 Kwa kuwezesha kupata mradi huo ambao utasaidia kupunguza tatizo la maji katika eneo Hilo.

Diwani wa kata ya Luhanga wilaya ya Mbarali Baraka Leteyo (aliyeshika maiki)akitoa maneno ya shukrani mbele ya viongozi wa kanisa na 21 mission
Sauti ya diwani wa kata ya Luhanga wilaya ya Mbarali Baraka Leteyo

Kwa upande wake mratibu wa mradi wa Tree project ndani ya mission 21 Thobias Teobadia amesema mradi huo umegharimu zaidi ya Tsh million 40 na mradi huo utasaidia kupunguza tatizo la maji katika jamii hiyo.

Sauti ya mratibu wa mradi wa Tree project ndani ya mission 21 Thobias Teobadia

Naye Mratibu wa Mission 21 hapa nchini Adrian Sweetmen amesema mradi huo utasaidia hasa wanawake ambao ndio wahanga wakubwa katika jamii, ambapo pia wameanzisha vitalu vya miti na kuazisha vikundi mbalimbali Kwa lengo la kuwainua kiuchumi.

Ameongeza kuwa mradi huo ni msaada kutoka Kwa mpenda maendeleo wa Uswiswi Bi Elizabeth.

Mratibu wa Mission 21 hapa nchini Adrian Sweetmen(kulia).
Sauti ya Mratibu wa Mission 21 hapa nchini Adrian Sweetmen

Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa KMT-JKM Mch Asulumenye Mwahalende ameushukuru mradi wa mission 21 Kwa kazi wanazoendelea kufanya ndani ya jamii na Kwa kanisa Kwa ujumla.

Pia amewataka wananchi wa Luhanga kumshukuru sana Mungu Kwa matendo makuu aliyowatendea ya kupata mradi huo, huku akiwataka kujitunza na kuilinda Ili iweze kuwasaidia wao na vizazi vijavyo.

Makamu mwenyekiti wa KMT-JKM Mch Asulumenye Mwahalende(wa pili kulia auto buluu) akikagua mradi wa miti unaotekelezwa na mradi wa 21 mission

Mradi wa mission 21 kwa kushirikiana na KMT-JKM Inaendeleza kampeni ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kumtua mama ndio kichwani.