Baraka FM

Moto wateketeza madarasa, nyaraka muhimu za shule Mbeya

21 October 2024, 08:18

Sehemu ya madarasa ya shule ya msingi jitegemee yakiendelea kuteketea kwa moto

Elimu ya uzimaji Moto inapaswa kuendelea kutolewa kwa wananchi ili kukabiliana na majanga ya Moto

Na Mwandishi wetu

Vyumba vitatu vya Madarasa na ofisi moja ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Jitegemee iliyopo Mji Mdogo wa Mbalizi Wilaya ya Mbeya, vimeteketea kwa moto mapema hii Leo huku chanzo Cha moto huo kikiwa bado hakijifahamika.

Moto huo unaodaiwa kuanza majira ya saa moja asubuhi umeteketeza kabisa ofisi ya Mwalimu mkuu pamoja na Mali zote ikiwemo nyaraka mbalimbali za shule, wanafunzi pamoja na hundi Kama anavyo tueleza Mwalimu mkuu wa shule hiyo.

Malongo sumuni ni mtendaji wa mtaa wa mlimareli, anasema moto huo ambao ambao unaonekana umetokana na hitilafu kwenye mfumo wa umeme umesababisha hasara Kwa kutekeleza kabisa vyumba vitatu vilivyokua vikitumiwa na wanafunzi, huku diwani wa kata ya Utengule Usongwe Yona Ntumjilwa akitoa pole kwa waliojeruhiwa wakati wa kuzima moto huo mara baada ya kutokea

Mtendaji wa mtaa wa mlimareli Malongo sumuni

Kamanda wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji na Mkoa wa Mbeya Mrakibu Malumbo Ngata amethibitisha kutokea kwa tukio la moto huo katika shule ya Msingi Jitegemee.

Kamanda wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji na Mkoa wa Mbeya Mrakibu Malumbo Ngata