Baraka FM

Vijana watakiwa kuwa wazalendo kwa taifa lao

20 October 2024, 19:54

Aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Tanzania Mh. Lazaro Nyarandu akisaini kitabu cha wageni baada ya kufika katika kituo cha Radio Baraka fm

Taifa lolote linategemea nguvu ya vijana hivyo kwa kutambua hilo mamlaka zimekuwa na wajihubwa kuwajenga vijana kuwa wazalendo.

Na Kelvin Lameck

Aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Tanzania Mh. Lazaro Nyarandu amewataka vijana kuwa wazalendo kwa kufanya mambo yatakayoleta umoja na mshikamano.

Mhe. Nyalandu amesema hayo leo wakati akizungumza kupitia kipindi cha Nuru ya Asubuhi kinachoruka Baraka Fm, kuelekea kongamano la vijana litakalofanyika Octoba 20 mwaka huu katika ukumbi wa Eden jijini Mbeya.

Ameongeza kuwa uzalendo unaanza na mtu binafsi hivyo kila mmoja aungane kuhakikisha anaitangaza nchi kwa kutangaza vitu vyenye mantiki badala ya kusemana vibaya.

Katika hatua nyingine amewaomba Watanzania kuendelea kujiandikisha katika daftari la Mpiga kura ili wapate nafasi ya kushiriki katika uchaguzi utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu na uchaguzi mkuu wa mwakani.

Akizungumza kwa niaba ya kikundi cha Samia Love, Ipyana Mwakyusa amesema vijana wote wanapaswa kushiriki kongamano hilo kwani watapata nafasi ya kujifunza mambo mbalimbali yenye tija kwa Taifa.