Vijana wa kanisa la Moravian washiriki mkutano na kujifunza neno la Mungu
14 October 2024, 13:41
Takribani siku nne vijana wa kanisa la Moravian wamekuwa na Mkutano wa kujifunza neno la Mungu.
Na Hobokela Lwinga
Vijana kati kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi wamehitimisha Mkutano wao mkuu wa Jimbo uliofanyika katika ushirika wa Mkwajuni mkoani Songwe.
Akizungumza na vijana hao wakati Wa kuwasilisha salamu za Jimbo, Katibu Mkuu kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi ndugu Israel Mwakilasa amesema lengo Mikutano hiyo ni kujiungamanisha na Mungu sambamba na kumshukru Mungu katika matendo makuu anayoyafanya kwa kila mtu na kanisa.
Sambamba na hayo Mwakilasa amewataka vijana hao kutunza amani ya kanisa na taifa kwa ujumla.
Akihubiri katika ibada ya kufunga mkutano huo katibu Wa wilaya ya Mbeya mch.Nuru Mwamahonje amesema vijana wanapaswa kumtumikia Mungu kwa kuachana na uovu unaotendeka duniani.
Aidha katibu wa idara kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mch.Abel Mbise amewataka vijana kuepuka mafundisho ya uongo yanayotolewa na baadhi ya watu wanaojiita watumishi Wa Mungu.
baadhi ya washiriki wa mkutano huo wamesema Mkutano huo umekuwa na faida kwani wamejifunza mambo mbalimbali huku wakilishukru kanisa kwa kuwezesha Mkutano huo.
Katika mkutano huo vijana hao wameweza kuonyesha vipawa mbalimbali ikiwemo usomaji Wa Biblia, kujifunza masomo ya uchumi, utandawazi ndoa pamoja na uimbaji.