Baraka FM

Watu 17 wajeruhiwa katika ajali Jijini Mbeya

8 October 2024, 00:05

Magari yaliyogongana uso kwa uso sae jijini Mbeya (picha na Ezekiel Kamanga)

Mapema Leo Kumeshuhudiwa Kutokea Kwa Jali Ya Masafa Marefu Sae Jijini Mbeya

Na Ezekiel Kamanga

Watu kumi na saba wamejeruhiwa baada ya mabasi mawili yanayofanya safari zake Mbeya-Arusha mali ya kampuni ya Kaplikon na basi jingine la kampuni ya Premier linalofanya safari zake Mwanza-Mbeya kugongana uso kwa uso eneo la Sae Jijini Mbeya.

Baadhi ya mashuhuda wamedai kuwa ajali hiyo imetokea wakati gari ndogo ikijaribu kuingia barabarani na wakati mabasi yakimkwepa ndipo yameweza kugongana.

Sauti za baadhi ya mashuhuda wa ajali

Malumbo Ngata ni Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mbeya amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo majira ya saa kumi na moja asubuhi.

Sauti ya Malumbo Ngata ni Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mbeya

Naye Rajab Guliku Mwenyekiti wa Usalama barabarani Mkoa wa Mbeya amewasihi madereva kuwa makini wanapokuwa barabarani.

Sauti ya Rajab Guliku Mwenyekiti wa Usalama barabarani Mkoa wa Mbeya

Majeruhi wote wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa Kanda Mbeya na hali zao zinatajwa kuendelea vizuri.