Jamii yashauriwa kumtegemea Mungu na kuachana na Imani potofu
7 October 2024, 23:11
Wakati matukio mbalimbali yakiendelea kutokea nchini sababu inatajwa kuwa watu kumuacha Mungu na kufanya vitendo Vya kishirikina.
Na Ezekiel Kamanga
Wakristo Duniani wametakiwa kukimbilia kwenye nyumba za ibada pia watumishi wawe faraja kwa waumini wao badala ya kutangatanga mitaani ambako hufundishwa imani potofu ambazo huliangamiza Kanisa na Taifa kwa ujumla.
Wito huo umetolewa na Mchungaji Christopher Mwamzanya Mswima wa Kanisa la International Pentecostal Holiness Church Naioth Worship Center (Kituo cha Makimbilio)lililopo Mwambene Kata ya Mwakibete Jijini Mbeya.
Amesema Kanisa linapaswa kuona aibu kwa kutotatua shida za watu kama ndoa na magonjwa.
Katika hatua nyingine Mchungaji Christopher Mwamzanya Mswima amewataka Waumini kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu kwani wasiposhiriki wasitoe lawama endapo watachaguliwa viongozi wasio waadilifu.
Baadhi ya waumini wameupokea vema ujumbe huo na kuahidi kuufanyia kazi.
Endapo Wakristo nchini wataungana kueneza imani ya kweli waumini watakuwa kimwili na kiroho sanjari na kudumisha amani nchini.