Baraka FM

Watu kadhaa wanahofiwa kufa, kujeruhiwa ajalini Mbeya

7 October 2024, 09:35

Wananchi wakilishuhudia gari ambapo limepata ajali mapema leo sae Jijini Mbeya

Jinamizi la ajali bado limeendelea kuutesa mkoa wa Mbeya kutokana na matukio hayo ambayo yametokea mfululizo hivi karibuni.

Na Ezekiel Kamanga

Ajali iliyohusisha mabasi mawili ya kampuni ya Kapricon Express na Premier Line yamegongana uso kwa uso eneo la Sae jijini Mbeya majira ya saa 12 asubuhi.

Idadi ya watu waliopoteza maisha na majeruhi wa ajali hiyo haijajulikana bado huku vikosi vya askari wa usalama barabarani na Jeshi la Zima moto na Uokoaji wamefika eneo la tukio na kusimamia zoezi la kuwaokoa majeruhi pamoja na kuyanasua magari hayo.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo chanzo cha ajali ni gari dogo lililotokea eneo la Mbeya Pazuri Social Club kuingia barabarani bila kuchukua tahadhari na kusambabisha mabasi haya kutafuta jinsi ya kulikwepa gari hilo na kugongana.

Jitihada za kumtafuta kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya ili kuthibitisha tukio hilo zinaendelea