Baraka FM

Askofu Pangani kuzindua ofisi za kanisa la Moravian wilaya ya Mbalizi

4 October 2024, 10:56

Muonekano wa mbele wa ofisi mpya za kanisa la Moravian wilaya ya Mbalizi.

Kanisa la Moravian Tanzania limekuwa na Utaratibu wa kuhahakisha majimbo na wilaya zake kuwa na makao makuu na kujenga ofisi bora ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa huduma za kiroho kwa ustawi wa kanisa.

Na Hobokela Lwinga

Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini magharibi wilaya ya Mbalizi imekamilisha ujenzi wa ofisi kuu za wilaya hiyo zilizojengwa Mtakuja mji mdogo wa Mbalizi halmashauri ya wilaya ya Mbeya.

Lengo la ujenzi wa ofisi hizo ni kusogeza huduma za kiroho na utendaji katika shirika zinazounda wilaya hiyo ya Kanisa na zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi na baba Askofu Robert Pangani jumapili hii ya October 06,2024.

Akizungumzia uwepo wa ofisi hizo Mwenyekiti wa wilaya ya Mbalizi kanisa la Moravian mchungaji Elika Samwanijembe amesema majengo ya ofisi hizo yamejengwa na kupambwa kwa rangi za kanisa ambazo ni nyeupe zenye kiashiria Cha Utakatifu na Rangi ya kijani inayowakilisha ustawi wa kanisa.

Mwenyekiti wa wilaya ya Mbalizi kanisa la Moravian mchungaji Elika Samwanijembe

Hata hivyo katibu wa wilaya ya Mbalizi kanisa la Moravian mchungaji Paul Mwampamba amesema ofisi hiyo imejitosheleza kwani ina ofisi mbalimbali za viongozi kuanzia mwenyekiti, katibu, uwakili pamoja na ukumbi wa mikutano.

katibu wa wilaya ya Mbalizi kanisa la Moravian mchungaji Paul Mwampamba

Ikumbukwe kuwa wilaya ya Mbalizi ni mjumuisho wa wilaya zinazounda Jimbo la kusini magharibi kanisa la Moravian lenye wilaya nne za Mbeya, Mbalizi, Mbarali na Chunya pamoja na mission ya Iringa.

Mwenyekiti wa kanisa la Moravian wilaya ya Mbalizi mchungaji Elika Samwanijembe(kulia) akiwa na Katibu wa wilaya hiyo mchungaji Paul Mwampamba (kushoto) wakikagua ofisi kuelekea katika uzinduzi October 06,2024.