Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi jiji la Mbeya wajengewa uwezo
30 September 2024, 15:34
Maandalizi kuelekea uchaguzi wa serikali mitaa ambapo tayari elimu imeanza kutolewa kwa wasaidizi wa wasimamizi wa uchaguzi huo.
Deus Mellah
Halmashauri ya jiji la Mbeya imetoa mafunzo kwa Wasimamizi Wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata kuhusu kanuni na taratibu za kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.
Akizungumza na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi huo msimamizi msaidizi wa halmashauri ya jiji la Mbeya Davis Mbembela amewataka wasimamizi hao kuzingatia yote wanayoelekezwa na kuwa wawazi.
Mbembela ameongeza kuwa wasimamizi hao watapitishwa kwenye maeneo ya uchaguzi ili wayafahamu sambamba na kuwajua wagombea wa nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huo.
Naye Ally Nunduma ambaye ni msimamizi msaidizi wa uchaguzi halmashauri ya jiji la Mbeya amesema wanaendesha mafunzo ya uchaguzi wa serikali za mitaa ili wananchi wapate elimu.
Amesema katika jiji la Mbeya kuna tarafa mbili, kata thelathini na sita na mitaa miamoja themanini na moja ambapo chaguzi huo utafanyika.
Akizungumza kwa niaba ya wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi waliopata mafunzo hayo Liliani Mwakitosi amesema watafuata kanuni na sheria za uchaguzi ambazo zimewekwa pamoja na kutenda haki kwa wananchi wote.