Wazee waziomba halmashauri kuwapatia ofisi kuendesha shughuli zao
29 September 2024, 17:03
Uwepo wa dawati la baraza la wazee kwa ngazi ya taifa, mkoa, wilaya na kata wazee wameomba serikali kuwapatia ofisi.
Na Ezra Mwilwa
Katika kuelekea kilele cha kuadhimisha siku ya wazee duniani tarehe 01 Oktoba, wazee mkoani Mbeya wamekutana kuadhimisha kilele hicho kwa ngazi ya mkoa katika viwanja vya Rwanda Nzovwe jijini hapa.
Katika maadhimisho hayo mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mh. Kanali Maulid Sulungu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Juma Homela amesema kama serikali wataendelea kuimarisha miundombinu ya afya pia kuelimisha jamii kuwalinda wazee kwani wana msaada mkubwa katika jamii.
Pia Sulungu amewakumbusha wazee na wananchi kuendelea kujiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa ikiwa n ipamoja na uboreshwaji wa daftari la mpiga kula.
Mwenyekiti wa baraza la washauri la wazee mkoa wa Mbeya amesema wao kama wazee wanaomba kupewa ofisi katika ngazi za wilaya na kata.
Naye mwakilishi kutoka Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya Kika Stigina amesema wao wanapokea bima za afya na kwa wale wazee ambao hawana bima za afya wanapokelewa nakupatiwa matibabu.