Baraka FM

Watu 11 wafariki 20 wajeruhiwa ajali nyingine Mbeya

28 September 2024, 00:06

Baadhi ya Wananchi wakishuhudia ajali (Picha na Hobokela Lwinga)

Wimbi la ajali limeendelea kuukumba mkoa wa Mbeya ambapo kwa mwezi wa tisa pekee zimetokea ajali tatu.

Na Hobokela Lwinga

Watu 11 wamefariki dunia baada ya gari lenye namba za usajili T.601 CFS Lori aina ya Mitsubishi Fuso walilokuwa wamepanda kupinduka leo September 27,2024 wakati likitokea Mbalizi kuelekea kwenye mnada katika Kijiji cha Jojo kilichopo Kata ya Santilya Mkoani Mbeya.

Taarifa iliyotolewa leo na Polisi Mbeya imesema waliofariki ni Wanaume wanane na Wanawake watatu huku Majeruhi wakiwa ni 20 (Wanaume 10 na Wanawake 10) ambapo chanzo cha ajali kimetajwa kuwa ni Dereva kushindwa kuchukua tahadhari kwenye mteremko na kusababisha gari kuacha njia na kupinduka.

Majeruhi bado wanaendelea kupatiwa matibabu katika Kituo cha Afya cha Ilembo huku Polisi wakiendelea kumsaka Dereva ambaye alikimbia muda mfupi baada ya ajali “Jeshi la Polisi linaendelea kutoa wito kwa Madereva kuendelea kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuacha tabia ya kupakia Abiria kwenye magari ya mizigo”