Baraka FM

Viongozi kanisa la Moravian Tanzania washiriki mkutano mkuu wa dunia

26 September 2024, 20:22

Katika kudumisha na kuendeleza Injili kupitia kanisa la Moravian duniani kunalifanya kanisa hilo kuwa na mikutano ya pamoja.

Na Hobokela Lwinga

Wenyeviti wa majimbo yanayounda kanisa la Moravian Tanzania wameshiriki mkutano Mkuu wa kanisa la Moravian duniani unaofanyika katika visiwa Vya Antigua nchini Marekani.

Katika mkutano huo umeanza September 26,2024 na utamalizika October 02,2024 na umehudhuriwa na wenye viti mbalimbali kutoka majimbo ya kanisa la Moravian duniani.

Aidha kutoka Tanzania wenyeviti waliohudhuria mkutano huo ni mwenyekiti kutoka Jimbo la kusini (Rungwe), Tabora, kusini magharibi(Mbeya),Jimbo la mashariki, Ziwa Tanganyika,Jimbo la Mbozi(Songwe), Jimbo la kasikazini pamoja na wenyeviti wa majimbo ya mission ikiwemo mission ya Iringa na Morogoro.

Katika mkutano huo zimewasilishwa ajenda mbalimbali ambazo zimejadiliwa kwa ajili ya mstakabali wa kanisa la Moravian duniani.