Vijana watakiwa kutumia nguvu zao kujiimarisha kiroho, kiuchumi
13 September 2024, 22:15
Mafaniko ya mwanadamu yanategemea nguvu ya uwekezaji alionao mtu na ili uweze kufanikiwa ni lazima ujiepushe na mambo ambayo yanaweza yakakufanya ukashindwa kufanikiwa.
Na Hobokela Lwinga
Vijana wametakiwa kutumia muda wao mwingi katika kumtumikia Mungu na kujiimarisha kiuchumi kwani umri wao ndio kipindi ambacho wanapaswa kutengeneza maisha yao ya kiroho na kimwili.
Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa wilaya ya Mbeya kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mchungaji Osia Mbotwa Leo September 13,2024 Wakati wa ufunguzi wa mkutano wa vijana kati wa wilaya hiyo unaofanyika katika ushirika wa ibala uyole ya kati Jijini Mbeya.
Mchungaji mbotwa ameongeza kuwa umri wa vijana unaruhusu kujishughulisha katika kazi yoyote ambayo inajitokeza mbele yake
Mwenyekiti huyo amewataka kutokuwa tegemezi kutegemea Mali za wazazi badala yake natafuta Mali zao
Pia amewataka kutafuta familia Zao kwa Utaratibu wa kanisani huku akiwashauri kuzaa watoto wengi ambayo wanaweza kuwa tegemeo katika familia zao.
Mkutano huo wa wilaya wa vijana kati ni miongoni mwa mikutano iliyo kwenye Utaratibu wa kalenda ya kanisa la Moravian Jimbo la kusini magharibi na utamalizika jumapili ya September 15,2024.