Baraka FM

Wachungaji 49 Moravian wapanda madaraja ya ushemasi, ukasisi

10 September 2024, 06:53

Baadhi ya wachungaji waliopandishwa madaraja.

Kanisa la Moravian Tanzania limekuwa na Utaratibu wa kuwapandisha ngazi wachungaji wake hii ikiwa ni moja ya sifa ya makanisa ya kiprotenstanti katika madaraja matatu yaani ushemasi, ukasisi na uaskofu.

Na Hobokela Lwinga

Askofu mstaafu wa Kanisa la Moravian Tanzania jimbo la kusini Lusekelo Mwakafwila amewataka wachungaji na Wakristo kwa ujumla kuwa chanzo cha kutunza amani kwenye maeneo yao ya huduma.

Wito huo ameutoa wakati akihubiri katika Ibada ya Mbaraka wa Wachungaji iliyofanyika katika Ushirika wa Lutengano Jimbo la Kusini Kanisa la Moravian lililopo halmashauri ya Rungwe Mkoani Mbeya.

Sauti ya Askofu mstaafu wa Kanisa la Moravian Tanzania jimbo la kusini Lusekelo Mwakafwila

Askofu Mwakafwila Amesema palipo na uwepo wa Mungu Pana amani hivyo kila mtu anawajibu wa kumtafuta Mungu aliyechanzo cha amani.

Sauti ya Askofu mstaafu wa Kanisa la Moravian Tanzania jimbo la kusini Lusekelo Mwakafwila
Katika picha (kushoto) ni Askofu Kenan Panja wa kanisa la Moravian Jimbo la kusini na (kulia) ni Askofu mstaafu wa Jimbo hilo Lusekelo Mwakafwila.

Kwa upande wake Askofu wa kanisa la Moravian Tanzania jimbo la kusini Kenani Panja amewataka Wachungaji hao kuutafakari utakatifu wa wito wa huduma waliyoitiwa ya kuchunga Kondoo.

Sauti ya Askofu wa kanisa la Moravian Tanzania jimbo la kusini Kenani Panja

Awali Mwenyekiti wa Halmashauri kuu ya Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini. Mch.Ezekiel Mwasamboma alimuomba Askofu kuwapandisha ngazi Wachungaji hao kwa kuwa wamekidhi vigezo vya kufikia madaraja hayo kwa mujibu wa katiba ya Kanisa la Moravian.

Maaskofu wakiwaweka wakfu baadhi ya wachungaji katika mbaraka ushirikani Lutengano
Sauti ya Mwenyekiti wa Halmashauri kuu ya Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini. Mch.Ezekiel Mwasamboma

Baadhi ya wabarikiwa wakila kiapo cha Uchungaji wamesema wako tayari kumtumikia Mungu na Kanisa huku wakiomba Mungu awasaidie katika kazi hiyo.

Sauti za Baadhi ya wabarikiwa wakila kiapo cha Uchungaji

Katika Mbaraka huo jumla ya wachungaji 49 wamebarikiwa 10 wakiwa katika ngazi ya ya ushemasi, huku ukasisi wkibarikiwa wachungaji 39.