Vijana watakiwa kutojihusisha na vurugu ndani ya kanisa
6 September 2024, 13:46
Ili kuwa na kizazi chenye maadili mema kanisa la Moravian limekuwa na Utaratibu wa kuratibu mikutano mbalimbali kwenye idara Zake ikiwemo vijana ili kuwafundisha kumjua Mungu.
Na Hobokela Lwinga
Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi limewataka vijana kuwa mstari wa mbele kumtumikia Mungu na kanisa kwa ujumla kwani kufanya hivyo ni kujitengenezea vizazi vyako Vya sasa na Vya badae.
Wito huo umetolewa Katibu mkuu wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi Wakati akifungua mkutano wa Jimbo wa idara ya vijana A ulioanza September 05,2024 na utahitimishwa katika ushirika wa Iwindi halmashauri ya Mbeya.
Katibu Mkuu Mwakilasa ameongeza kuwa vijana wanapaswa kutumia mikutano hiyo kujifunza na kuepuka migogoro isiyo na ya lazima kwani kufanya hivyo ni chukizo kwa Mungu.
Kwa upande wake mchungaji wa ushirika wa iwindi Yusuph Kapusi na Katibu wa wilaya ya Mbalizi kanisa la Moravian Poul Mwampamba wamelishukru Jimbo kwa kuona umuhimu mkutano huo kufanyika kwenye eneo lao.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo amesema wanatarajia kujifunza mambo mbalimbali akiwemo mafundisho ya neno la Mungu na uimbambaji huku wakilishukru kanisa kwa kuwa na Utaratibu wa kuwakutanisha vijana kutoka maeneo mbalimbali.
Mkutano huo umehudhuriwa na wageni Wengine akiwemo Katibu wa idara ya vijana Jimbo la kusini magharibi mchungaji Abel Mbise pamoja na makatibu wa wilaya zote nne zinazounda Jimbo la kusini magharibi.
Pamoja na wageni hao mgeni kutoka ujerumani bw.Florian amekuwa sehemu ya wageni walioshiriki ufunguzi huo.