Watu 9 wafariki,18 wajeruhiwa ajalini Mbeya
5 September 2024, 09:34
Basi lililokuwa linatokea Sumbawanga kuelekea Ubaruki na lilipofika eneo la Kijiji cha ya Mbarali kwenye kona kali dereva alishindwa kulimudu na kusababisha ajali.
Na Hobokela Lwinga
Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mbeya Lina Mshikilia Dereva Alfredy Baharia Mwidunda [50] Mkazi Wa Ubaruku Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya Kwa Tuhuma Za Kusababisha Ajali Ya Gari Iliyoua Watu 9 Na Wengine 18 Kujeruhiwa Mkoani Humo.
Kwa Mujibu Wa Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mbeya Benjamin Kuzaga, Septemba 3 Mwaka Huu Katika Barabara Kuu Ya Mbeya –Njombe Gari Hilo Lenye Namba T.896 DHK Aina Ya Yutong Basi La Abiria Mali Ya Kampuni Ya Shari Line Lililokuwa Likitokea Sumbawanga Mkoani Rukwa Kuelekea Ubaruku Wilaya Ya Mbarali Mkoani Humo Liliacha Njia Na Kugonga Ukuta Wa Gema Na Kusababisha Vifo Hivyo Na Majeruhi.
Kamanda Kuzaga Amesema Kuwa Chanzo Cha Ajali Hiyo Ni Uzembe Wa Dereva Wa Basi Hilo Kushindwa Kulimudu Gari Hilo Kwenye Kona Kali Na Kusababisha Kuacha Njia Na Kutumbukia Korongoni Na Kugonga Gema.
Vile Vile Kamanda Huyo Wa Polisi Mkoa Mbeya Amesema Dereva Wa Basi Hilo Anaendelea Kupatiwa Matibabu Katika Hospitali Ya Misheni Chimala Akiwa Chini Ya Ulinzi Wa Polisi Huku Miili Ya Marehemu Ikihifadhiwa Hospitali Ya Misheni Chimala Na Majeruhi Wanapatiwa Matibabu Hospitali Ya Rufaa Kanda Ya Mbeya Na Misheni Chimala.
Katika Hatua Nyingine Jeshi La Polisi Mkoani Humo Limetoa Wito Kwa Madereva Kuwa Makini Na Kuzingatia Sheria, Alama Na Michoro Ya Usalama Barabarani Ili Kuepuka Ajali Zinazoweza Kuepukika.