Wazazi waomba chakula shuleni kizingatie usafi
4 September 2024, 17:14
Ulaji wa chakula shuleni umeongeza ufaulu kwa wanafunzi wengi, hivyo wanafunzi wanapoandaliwa chakula inapaswa kuwepo na Mazingira ya usafi ili kuwaepusha na magonjwa ya tumbo ikiwemo kuhara.
Na mwandishi wetu
Baadhi ya wazazi na walezi jijini Mbeya wamewataka walimu kuwasimamia kwa ukaribu uandaaji wa vyakula vya watoto mashuleni katika mazingira ya usafi ili kuepuka changamoto za kiafya kwa watoto hao.
Wakizungumza na Dream Media wazazi hao wamesema kuwa ni vyema watoto wao wakapata chakula bora wawapo shuleni kutoka kwa wapishi ikiwa ni pamoja na usafi wa miili yao na mazingira
Benson Sanga Mwenyekiti wa maafisa lishe Tanzania amesema mtoto kupata chakula shuleni husaidia kuongeza ufaulu na kupunguza utoro jambo ambalo ndio lengo la kila mzazi
Hata hivyo afisa huyo amewaasa waandaaji wa vyakula mashuleni pamoja na kamati zao kuandaa chakula bora kwa kuzingatia lishe ili kuepukana na changamoto za kiafya kwa watoto.