Baraka FM

MNEC Mwaselela aanza rasmi ziara Chunya, kukagua miradi ya maendeleo

2 September 2024, 23:22

MNEC Ndele Mwaselela baada ya kuwasili wilayani Chunya akisaini kitabu Cha wageni katika ofisi za chama(picha na Ezra Mwilwa)

MNEC Mwaselela amekutana na wajumbe wote wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya na viongozi wa jumuiya zote za Chama Cha Mapinduzi wilayani Chunya.

Na Ezra Mwilwa

MNEC Mwaselela amepokea Taarifa za Miradi Iliyotekelezwa na Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wakati alipofanya ziara yake wilayani Chunya.

MNEC Mwaselela akizungumza na wananchi wa Chunya(picha na Ezra Mwilwa)

Miradi hiyo ni pamoja na uwekaji wa Taa za barabarani uboreshwaji wa Miundombinu ya Afya, Mradi wa maji, Ujenzi wa stendi ya mabasi .

Mwisho MNEC Mwaselela amempongeza Mbunge wa Jimbo la Lupa Mheshimiwa Masache Kasaka na baraza la madiwani kwa kuendelea kuwapambania wananchi wa wilaya ya Chunya.

Wananchi wa Chunya wakiwa kwenye mkutano wa MNEC Ndele Mwaselela (picha na Ezra Mwilwa)