Baraka FM

Wafanyabiashara soko kuu Mwanjelwa Mbeya walalamikia soko kudolola

2 September 2024, 18:33

Muonekano wa soko Kuu Mwanjelwa Mbeya(picha na mtandao)

Soko kuu la Mwanjelwa jijini Mbeya limekuwa na changamoto ambazo zimekuwa zikilalamilikiwa kwa muda mrefu ikiwemo kukukosa wateja wa kununua bidhaa kwani wengi wao wamekuwa wakitumia masoko ya nje ya soko.

Na Hobokela Lwinga

Wafanyabiashara wa soko Kuu la Mwanjelwa Jijini Mbeya wamelalamikia kukosa wateja katika soko hilo kutokana na watu wengine kufanyia biashara zao maeneo yanayolizunguka soko hilo.

Wakizungumza Na Baraka fm radio wafanyabiashara hao wamesema hali hiyo inasababisha kushindwa kuuza bidhaa Zao ndani ya soko hilo wakisema wateja huishia nje na kushindwa kuingia ndani jambo ambalo linawapa hofu ya kupoteza mitaji yao .

Katibu Wa Soko Kuu la Mwanjelwa Abinala Mwakatumbula amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo ambayo imekuwa ikiwakabili kwa muda mrefu, ambapo amewataka wafanyabiashara hao kuwa na subira wakati wanasubiri maelekezo mengine.

Kwa upande wake Mkurugenzi Wa halmashauri ya jiji la mbeya John Nchimbi amewataka wafanyabiashara hao kuendelea kuiamini serikali wakati utaratibu mzuri ukifanyika kwenye soko hilo.