Askofu Pangani awataka wazazi kuombea watoto ili wamjue Mungu
1 September 2024, 11:03
Kanisa la Moravian kupitia taratibu zake katika utumishi limeweka ukomo wa miaka 60 kwa wachungaji kutumika kwenye nafasi hiyo.
Na Ezekiel Kamanga
Askofu Robert Pangani wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi amewataka Watanzania kuwaombea watoto ili wamjue Mungu hali hiyo italeta amani ndani ya nyumba, Kanisa na Taifa kwa ujumla.
Ameyasema hayo katika ibada maalumu ya kumuaga Mchungaji Anyandwile Kajange ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wilaya ya Chunya ambaye amefikia muda wa kustaafu.
Aidha amewataka Waumini kuwa na umoja kuacha marumbano yasiyo na tija yanarudisha nyuma maendeleo ya Kanisa na amesema pamoja na wito wa uchungaji Kanisa halitasita kuchukua hatua za kinidhamu.
Katika hatua nyingine amewataka Wamoravian kujitoa zaidi ili Kanisa liweze kujitegemea zaidi.
Pia amempongeza Mchungaji Anyandwile Kajange kwa ujenzi wa mpya ya ofisi ya Wilaya ya Chunya hivyo Jimbo linafikiria kuanzisha misheni ikiwa ni hatua ya kuanzisha Jimbo.
Kwa upande wake mch.Anyandwile Kajange amesema kwenye utumishi wake amepitia kipindi tofauti vya utumishi huku akisema katika nafasi ya uchungaji ametumika kwa miaka 19.