Baraka FM

MNEC Mwaselela na Viongozi wengine wauaga Mwenge wa Uhuru.

31 August 2024, 23:04

Mjumbe wa harimashauri mkuu ya chama cha pinduzi Ndele Mwaselela(aliye shika Mwenge wa Uhuru) akiongoza viongozi wengine wa mkoa wa Mbeya kuuga Mwenge wa Uhuru.

Baada ya Mwenge wa Uhuru kukagua na kizindua miradi Mbalimbali mkoani mbeya, umeagwa rasmi kuelekea mkoani Songwe.

Na Ezra Mwilwa

Mjumbe Wa Halmashauri Kuu Ya CCM Taifa NEC Ndugu Ndele Mwaselela Amewaongoza Wajumbe Wa Kamati ya Siasa Mkoa Wa Mbeya pamoja na Viongozi wa CCM Ngazi ya Wilaya Katika Kuuga Mwenge wa Uhuru na Mkoani Songwe, Ukitokea Wilaya ya Mbeya Katika Halmashauri ya Mbeya mjini.

Mwenge wa Uhuru ukiagwa mkoani Mbeya (picha na Ezra Mwilwa)

Ikumbukwe Mwenge wa Uhuru Ulipokelewa Mkoani Mbeya Ukitokea Mkoani Tabora, Na Kukimbizwa Wilaya Na Halmashauri Zote Ndani ya Mkoa Wa Mbeya na Kukagua Miradi MbaliMbali ya Maendeleo.