Askofu Pangani ashiriki ibada ya kuaga mwili wa marehemu Mwasuka
31 August 2024, 09:15
Kuishi duniani ni matakwa ya Mungu kwani vitabu vitakatifu vinatueleza wazi kuwa duniani si makazi ya kudumu kwa kiumbe chochote hai akiwemo binadamu, hivyo Mungu kupitia vitabu yake vitakatifu vinatuelekeza kutenda mambo mema ambayo si chukizo kwake ili baada ya kutwaliwa tuweze kuurithi ufalme wake.
Na Hobokela Lwinga
Askofu kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi Robert Yondam Pangani ameshiriki ibada ya kuaga mwili wa Mama mzazi wa Mchungaji Suma Mwankuga marehemu Mele Lusako Mwasuka ambaye pia ni mama mkwe wa askofu Lawi Mwankuga wa Jimbo la mashariki.
Ibada ya kuaga mwili wa marehemu imefanyika katika kanisa la moravian Tanzania Jimbo la kusini ushirika wa Rungwe august 29,2024.
Katika ibada hiyo viongozi mbalimbali wa majimbo ya kanisa la Moravian wamehudhuria akiwemo askofu Kenan Panja wa Jimbo la kusini(Rungwe) ambaye pia ni makamu askofu kiongozi kanisa la Moravian Tanzania, askofu Lawi Mwankuga wa Jimbo la mashariki(Dar es salaam),askofu mstaafu Jimbo la kusini Lusekelo Mwakafwila.
Viongozi wengine waliohudhuria ibada hiyo ni Katibu Mkuu kanisa la Moravian Tanzania mch.David Mgombele, mwenyekiti wa kanisa la moravian Jimbo la kusini Mch.Ezekiel Mwasamboma,Mwenyekiti wa kanisa la moravian Jimbo la mashariki mch.Gelard Simtengu,Katibu Mkuu wa kanisa la moravian Jimbo la kusini magharibi ndugu Israel Mwakilasa pamoja na viongozi wenyeji Jimbo la kusini akiwemo makamu mwenyekiti Jairy sengo na Katibu Mkuu Stephen Mwaipopo.
Marehemu Mele Lusako Mwasuka amezikwa katika halmashauri ya Rungwe august 29,2024, Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina lake Lihimidiwe.