Baraka FM

Wananchi Kyela wanufaika na mradi wa maji

28 August 2024, 23:05

Kyela wanufaika na mradi wa maji ulio zinduliwa na Mwenge wa Uhuru(picha na Ezra Mwilwa)

Wakazi wa kata Kijiji Cha Lema kata ya Busale Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya baada ya kukumbana na changamoto ya maji kwa mda mrefu hatimaye mradi mkubwa umejengwa na kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru.

Na Ezra Mwilwa

Kinamama kutoka kata Kijiji Cha Lema kata ya Busale Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya wameshindwa kujizuia na kulala chini baada ya mwenge wa Uhuru kuzindua mradi wa maji kijijini hapo na kupata maji Safi Kwa mara ya kwanza.

Wamesema Kwa muda mrefu wamekua wakifuata maji ya mto Kwa umabali wa zaidi ya maili kumi na kutumia maji hayo yasiyo salama kwao ambayo yamekua yakiwasababishia wananchi kqenye Kijiji chao na Kata Kwa ujumla kupata magonjwa ya mlipuko mara Kwa mara ikiwemo kipindupindu.

Baadhi ya viongozi wa wilaya ya Kyela wakiwa katika mradi wa maji(picha na Ezra Mwilwa)

Mhandisi Tanu Deule ni meneja wa wakala wa maji safi vijijini RUWASA, amesema mradi huo umeztumia zaidi ya millioni 300, na ulitakiwa kukamilika mwezi November mwaka Jana lakini ukashindikana kutokana na sababu mbalimbali na Sasa umekamilika na kuanza kutoa huduma Kwa wananchi zaidi ya Elfu Tano