Wananchi wahimizwa kutunza miundombinu ya barabara Kyela
28 August 2024, 17:43
Mwenge WA Uhuru unaendeleaje kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika halmashauri ya wilaya ya Kyela mkoani Mbeya
Na Hobokela Lwinga
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 Godfrey Mnzava Pamoja na timu yake ya Vijana Sita wamewaasa Wananchi hasa Madereva Kuitunza na Kunitumia kwa Matumizi Sahihi Barabara ya community yenye urefu wa Mita 380 inayopatikana Kata ya Mwananyanga na Mbugani Halmashauri ya Wilaya ya Kyela.
Ameyasema hayo Wakati akiikabua na kuizindua Barabara hiyo wakati akiwa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela ikiwa ni mwendelezo wa Zoezi la kukimbiza Mwenge Wa Uhuru Kitaifa 2024 Mkoani Mbeya
Kutoka kwa Wakala wa Barabara za Vijijini na mijini TARURA inasema Mradi huo unaotekelezwa na Mkandarasi wa Baasi General supplies Limited ulipangiwa Kutekelezwa kwa Bajeti ya Sh:337,128,446.70 Kutoka kwenye Chanzo Cha Fedha Cha Tozo ya Shilingi 100 kwa Lita ya Mafuta(Fuel Levy)
Kwa budget ya Mwaka wa Fedha 2023/2024.
Fedha zilizopokelewa kwa ajiri ya Ujenzi wa Barabara hiyo hadi Sasa ni Shilingi 100,233,500.00 sawa na asilimia 29.73 na ulipangwa Kumalizika tarehe 18/05/2024 ingawa muda wa Kumalizika uliongezwa kutokana na Changamoto ya Mvua kubwa zilizonyesha wakati huo.
Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mh:Josephine Manase amesema Kipindi Cha Masika hali ilikuwa mbaya na Changamoto kubwa kwa Wakazi wa mahali hapo hasa kupata huduma za upitaji hali iliyosababisha baadhi ya Shughuli za Wananchi za kiuchumi Kukwama.
Ameongeza kuwa Uwepo wa Barabara hiyo imekuwa ni faida saana Kwa Wananchi wa Kyela hivyo Viongozi wa Mwenge wampelekee Salamu Mh: Rais kuwa Jambo alilolifanya ni Kubwa na ni alama tosha kwa Wanañchi wa Halmashauri hiyo.