Baraka FM

Mwanaume ajinyonga kwa kutumia shuka Mbeya

28 August 2024, 15:38

Mfano wa picha ya mwanaume aliyejinyonga(picha na mtandao)

Maisha yana changamoto nyingi ambapo husababisha baadhi ya watu kuwa na msongo wa mawazo, hali hiyo husababisha wengine kujiondoa duniani kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujinyonga na wengine kunywa sumu.

Na Flora Godwin

Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Lugano Mwamajuja mkazi wa Inyala Iyunga jijini Mbeya amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia shuka akiwa nyumbani kwake.

Wakizungumza na kituo hiki baadhi ya majirani na mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kusikitisha na kifo hicho kwani marehemu hajaacha ujumbe wowote ulio sababisha yeye kuchukua maamuzi hayo magumu.

Aidha wananchi hao wamesema ni vizuri watu wawe wanaomba ushauri au kushirikisha watu wengine juu ya changamoto wanazopitia kwani kufanya hivyo kutawasaidia kupunguza msongo wa mawazo.

Sauti za baadhi ya majirani na mashuhuda wa tukio

Akizungumzia tukio hilo Mwenyekiti wa mtaa wa Inyala Nelson Mahena amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mpakasasa hawaelewi sababu za kijana huyo kuchukua uamuzi mgumu kujinyonga.             

Mahena amewataka wanachi wa mtaa wa inyala kuwa watulivu huku viongozi wa mtaa wakitafuta ufumbuzi wa matujkio hayo  .

Sauti ya Mwenyekiti wa mtaa wa Inyala Nelson Mahena