Vijana watakiwa kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali
26 August 2024, 17:14
Utekelezaji wa Mradi huu Umefikia asilimia 30 ambapo Jumla ya Sh. 25,410,000 zimetumika kwaajiri ya Ununuzi wa Vifaa vya Ujenzi, Gharama ya fundi, Ununuzi wa Udongo na Ununuzi wa trey la kuoteshea Mbegu.
Na Hobokela Lwinga
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Wa Uhuru 2024 Ndg: Godfrey Mnzava amewataka Vijana Kuzitumia Vyema fursa za kujikwamua Kiuchumi zinazotolewa na Serikali kupitia Taasisi za Umma na Binafsi na kuepuka tabia za kulalamika kwa Madai ya Kwamba Maisha ni Magumu.
Mnzava ameyasema hayo Wakati akitembelea na kuzindua Mradi wa Kitalu Nyumba Cha kuotesha miche ya Mboga na Matunda kama Nyanya na miti ya matunda ulioanzoshwa na Kikundi Cha Vijana kiitwacho MAKIA Youth Group Mwaka 2024 kikijishughulisha na Utoaji Huduma kwa Wakulima, Ushauri na utunzaji wa Mazingira katika halmashauri ya Mbarali mkoani Mbeya.
Taarifa ya MAKIA imesema Gharama za Mradi wa Kitalu Nyumba mpaka unakamilika ni TSH. 99,410,000 kutoka kwenye kiasi Cha Sh. 25,410,000 ambacho ni Jumla ya Mapato yaliyopatikana kutokana na Mkopo wa Milioni Tano walizoomba Wahusika Kutoka Bank ya Vision Fund na Milioni 8 zilizochangwa na Wanachama wenyewe.
Hata hivyo Katika kuendelea kujiimarisha na kujitanua zaidi Kikundi kimeomba Mkopo wa Shilingi 74,000,000 Kutoka Halmashauri kupitia Mfuko wa Wanawake Vijana na wenye Ulemavu.
Ombi hili la Kupatiwa Mkopo limepokelewa Vyema ambapo Kiongozi wa Mbio za Mwenge ameiomba Halmashauri ya Mbarali Zoezi la Utoaji Mikopo litakapoanza Vijana hao waangaliwe katika Namna ya kupatiwa hitaji lao.
Mwenge wa Uhuru 2024 uliobeba Kauli mbiu ya Tunza Mazingira Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa leo Tarehe 26 August uko Wilayani Mbarali na Tarehe 27 utakuwa Wilayani Kyela.