Baraka FM

Mwenge wa Uhuru kuzindua miradi yenye thamani ya bilioni 39.8 mkoani Mbeya

24 August 2024, 12:12

Wananchi mkoani Mbeya wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuupokea mwenge wa Uhuru pindi utakapo pita kwenye maeneo yao ukizindua miradi mbalimbali.

Na Hobokela Lwinga

Mwenge wa Uhuru umepokelewa mkoani Mbeya kutoka mkoani tabora ambapo Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Rodrick Mpogolo amepokea Mwenge huo Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Cde: Juma Z. Homera Kutoka kwa Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Kata ya Kambikatoto Halmashauri ya Wilaya ya Chunya tayari kwaajiri ya kukimbizwa Mkoani Mbeya.

Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Rodrick Mpogolo(kulia) akiwa tayari kwa mapokezi ya mwenge

Katika upokeaji wa mwenge huo wageni mbalimbali wamehudhuria ikiwemo Viongozi na wananchi kutoka kata jirani za halmashauri ya Chunya.

Mwenge Wa Uhuru ukiwa Mkoani Mbeya Utakimbizwa Kilomita 1171.16 Wilaya Tano na Halmashauri zote saba na utatembelea,utakagua na kuzindua Miradi 56 yenye thamani ya Bilioni 39.8.