Baraka FM

Wanahabari Mbeya wanolewa kuandika habari za rushwa kuelekea uchaguzi

22 August 2024, 16:37

Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa mbeya Maghela Nyimbo akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari Mbeya (picha na Hobokela Lwinga)

Uchaguzi ni moja ya nyanja inasababisha uwepo wa maendeleo ,kwani inatoa fursa ya kupata viongozi waliobora na wanao weza kuwa sababu ya kuchochea maendeleo kwenye jamii.

Na Hobokela Lwinga

Katika kuelekea katika uchaguzi serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025 taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU)Mkoa wa mbeya imetoa mafunzo kwa waandishi wa habari mkoani humo ili kuwajengea uelewa wa kuandika habari na kuwaelemisha wananchi kuepuka kupokea na kutoa rushwa.

Akizungumza na waandishi hao wakati akiwasilisha mada mkuu wa TAKUKURU mkoa wa mbeya Maghela Ndimbo amesema waandishi wa habari wanamchango mkubwa wa kutoa elimu kupitia vipindi wanavyofanya kwenye vituo vyao vya kazi.

Maghela Amesema lengo la serikali ni kuhakikisha wananchi wanakuwa na maendeleo bora na endelevu kwa kutambua kwamba rushwa ni adui wa maendeleo.

Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa mbeya Maghela Nyimbo(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya mkuu wa TAKUKURU mkoa wa mbeya Maghela Ndimbo

Aidha mkuu huyo ametaja sababu zinazosababisha uwepo wa rushwa kwenye jamii ni mmonyoko wa maadili,wananchi kutofahamu haki na wajibu wao katika huduma za jamii,tamaa,muundo wa maisha na ubinafsi huku akitaja madhara ya rushwa ikiwa ni pamoja na kukosa maendeleo mbalimbali.

Sauti ya mkuu wa TAKUKURU mkoa wa mbeya Maghela Ndimbo

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema, mafunzo hayo yamewapa mwanga wa namna yakutoa taarifa sahihi kwa wananchi wawapo katika utekelezaji wa majukumu yao.

Waandishi wa habari wakifuatilia mafunzo wakati mkuu wa TAKUKURU Mbeya Maghela Nyimbo [aliyesimama)akiwasilisha Masa(picha na Hobokela Lwinga).
Sauti za baadhi ya washiriki wa mafunzo