Baraka FM

Naweni mikono, tunza mazingira kuepuka maambukizi ya ugonjwa wa nyani

16 August 2024, 22:42

Mganga Mkuu mkoa Wa Mbeya Dkt. Elizabeth Nyama

Wakati serikali ikiendelea na mapambano ya ugonjwa wa nyani ulizuka katika baafhi ya nchi ikiwemo zile za jumuiya ya Afrika mashariki wananchi wanapaswa kuunga jitihada hizo na kuchukua tahadhali.

Na Hobokela Lwinga

Wananchi mkoani Mbeya wametakiwa kuchukua fahadhari dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa homa ya Nyani kwa kuwa na utamaduni wa kunawa mikono na kufanya usafi wa mazingira ili kujilinda zaidi.

Hayo yamezungumwa na mganga Mkuu mkoa Wa Mbeya Dkt. Elizabeth Nyema wakati akifanya mahojiano maalumu na na Baraka fm ambapo amesema kwasasa hakuna maambukizi yoyote yaliyoripotiwa ila Serikali inaendelea kutoa elimu juu ya kujikinga na ugonjwa huo.

Aidha Mganga Mkuu huyo amesema Serikali inafanya jitihada mbalimbali za kuzuia maambukizi ya homa ya nyani Mkoani humo ikiwemo kufanya vikao vya ujirani mwema na nchi jirani ili kujadili namna ya kukabiliana nao.

Nao baadhi ya wananchi Jijini Mbeya wamesema kwamba hawana elimu ya kutosha juu ya ugonjwa huo hali inayosababisha kuwepo kwa hofu vile vile kukumbana na upotoshwaji juu ya maradhi hayo.