Baraka FM

Milioni 37 zapatikana ujenzi jengo la kuabudia Moravian Jimbo la Kusini

13 August 2024, 17:46

Askofu Kenani Panja (kulia) akiagana na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera (kushoto) baada ya kumalizika kwa ibada ya harambee katika Ushirika wa Mahenge.

Taasisi za dini zimekuwa na mchango mkubwa nchini katika kudumisha amani na upendo hali hiyo imekuwa kichocheo kikubwa kwa viongozi wa serikali kuwa karibu katika kuchochea maendeleo ya taasisi hizo na taifa kwa ujumla.

Na Mwandishi wetu.

Makamu Askofu wa kanisa la Moravian Tanzania na Askofu wa kanisa la Moravian jimbo la kusini Kenani Panja ameongoza ibada ya harambee ya UJENZI wa nyumba ya kuabudia ya Ushirika wa mahenge unaopatikana katika halmashauri ya wilaya Rungwe mkoani Mbeya.

Katika harambee hiyo zimepatika jumla ya shilingi million thelathini na Saba hivyo kupatikana kwa fedha ni kiashiria cha kuanza ujenzi huo ndani ya Ushirika huo.

Aidha katika harambee hiyo imehudhuriwa na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera ambaye amemwakilisha Waziri Mkuu kassimu Majaliwa.

Katika Hotuba yake ambayo ameisoma kwaniaba ya Waziri Mkuu RC Homera Amesema Tanzania inajali na kuthamini sana Kazi inayofanywa na Taasisi za Kidini ikiwemo Kanisa la Moravian katika kudumisha Amani na Upendo zaidi sana katika Malezi ya Kimwili na Kiroho kwa Watu wa Rika zote.

“Rais wetu Mpendwa ametuma Salamu kwenu na Yeye ndiye aliyenituma Kuja na kushirikiana nanyi katika jambo hili jema na lenye Baraka tele, Mh: Rais amenituma Niwambie kuwa Serikali Iko nanyi bega kwa bega itaendelea kuwasapoti na kuwathamini maana Mchango wenu kwenye hili Taifa ni Mkubwa Mnoo” Ameyasoma RC Homera.