Pareto yawanufaisha wakulima,familia ya Mbwelo yapata padri
24 July 2024, 10:00
Kilimo cha pareto kimekuwa na manufaa makubwa kwa wakulima wengi, kutokana frusa hiyo kampuni ya uzinduzi wa pareto PCT Imekuwa ikihamasisha wakulima kuchangamkia kilimo hicho kwa kuwa patia wakulima mbegu bure na kulipa thamani zao hilo kwa kununua kwa Bei nzuri yenye manufaa kwa wakulima.
Na Flora Godwin
Kampuni ya ununuzi wa zao la Pareto (PCT) imeiomba serikali kufanya tathimini ya bei mpya ya zao la Pareto kwa ajili ya manufaa ya wakulima na makampuni ya ununuzi.
Ombi hilo limetolewa na Afisa Pareto mkoa wa Mbeya na Songwe Musa Malubalo katika tafrija ya kumpongeza mtoto wa moja ya mawakala wa kampuni hiyo Maiko Mbwelo baada ya kuhitimu na kupata nafasi ya kuwa Padri katika kanisa katoliki.
Malubalo ameiomba serikali kudhibiti vishoka ambapo amesema moja ya changamoto wanayokumbana nayo ni tatizo la kuwepo kwa vishoka ambao wanashusha thamani ya zao hilo.
Naye Maiko Mbwelo zao la Pareto linamsaidia kukuza uchumi wake kwani mpaka sasa anaweza kusomesha watoto alio nao.
Naye mmoja wa wakulima wa Pareto amesema changamoto wanayokumbana nayo ni uwepo wa makampuni yasiyotambulika yanayofanya ununuzi wa Pareto kinyamela.