Rais Samia apongezwa kwa utekelezaji miradi ya maendeleo Mbeya
23 July 2024, 10:50
Viongozi wa Serikali wameletwa ili kuiponya Miili ya Watu wakiwemo Viongozi wa dini ndio maana vitabu vya dini vinasisitiza kutii mamlaka iliyojuu ya mtu.
Na Hobokela Lwinga
Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Rodrick Mpogolo amekutana na Kufanya Mazungumzo na Prophet (Nabii)Philbert Paschal Kiongozi wa Makanisa ya CLJN Tanzania na Afrika Leo Ofsini kwake baada ya kutembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa Lengo la kuja kusalimia.
Katika Mazungumzo Yao Nabii Amesema mbali na kuja kutangaza Ukuu wa Mungu Mkoani Mbeya lakini pia amekuja kusaidia Wakazi wa Mbeya hasa wale Wenye Matatizo ya Kiroho na atakuwa na huduma ya seminar na kumsikiliza Mtu Mmoja Mmoja.
Hata hivyo Nabii Philbert ameupongeza Uongozi wa Dkt: Samia Suluhu Hassan Rais wa Tanzania kwa kuendelea kuboresha Miundombinu Mbalimbali Mkoani Mbeya na hii ni Baada ya kufurahishwa na umahili na Ubora wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya mara baada ya Kuwasili hapo.
Kwa Upande wake Katibu Tawala Mkoa amempongeza Nabii kwa Kusudio lake zuri la kufika Mbeya na Kutoa Wito kwa Viongozi wa Dini kuendelea kufundisha na kukemea Vitendo vinavyoendelea katika Jamii yetu hasa vile visivyo na Maadili kwa Vijana wa Kitanzania
” Kwakweli Mnafanya Kazi Nzuri sana Sisi Viongozi wa Serikali tunatambua sana Mchango wenu Ombi langu Endeleeni kuwasaidia Vijana kuwajenga na kuwalea katika Maadili Mema na Msisite kukemea na kuonya pale mnapoona Mmomonyoko wa Maadili ukizidi kushamili katika Jamii yetu” Amesema Mpogolo aliyeonesha kuguswa na Ugeni huo
Awali kabla ya kukutana na Katibu Tawala Nabii Philbert alikutana na Kufanya Mazungumzo na Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Bwana:Said Juma Madito na Kuzungumza Mambo kadha wa kadha na Kisha kufanya Maombi.
Baada ya Maongezi ya Muda kidogo Nabii aliongoza Maombi ya Kuuombea Mkoa wa Mbeya kadharika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa chini ya Juma Zuberi Homera(RC) na Watumishi wote wa Ofisi hiyo Maombi ambaye Rodrick Mpogolo(RAS) alishiriki Vyema.