UWSA Mbeya kuongeza mtandao wa maji taka
19 July 2024, 17:29
Na Sifael Kyonjola
Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mkoa wa Mbeya imepanga kuongeza mtandao wa maji taka na kukarabati ili kuwafikia wateja wengi zaidi.
Hayo yamesemwa na kaimu meneja wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mkoa wa Mbeya mwandishi Samwel Mmakasa wakati akizungumza na kituo hiki juu ya uboreshaji wa miundo mbinu ya maji taka.
Mmakasa amesema mamlaka hiyo itaendelea kuboresha mifumo ya maji taka ambayo imeenea kwa asilimia 14 na una urefu wa kilomita 138 kjwa wakazi wa jiji la Mbeya.
Kwa upande wake afisa uhusiano wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mkoa wa mbeya Neema Stanton amesema wanakabiliana na changamoto ya wizi wa mifuniko ya chemba pamoja na utupaji wa taka ngumu katika chemba hizo.
Mmoja wa madiwani wa jiji la Mbeya Henry Mwangambaku amesema wananchi wanatakiwa kuitumia vizuri mifumo ya maji taka ambayo imepunguza gharama za uchimbaji wa mashimo ya vyoo.