Baraka FM

Wahitimu vyuo watakiwa kutumia elimu zao kukabiliana na ukatili

16 July 2024, 20:20

Kila Jambo linalopaswa huwa linakuwa na mwisho, hata kwenye suala la elimu nalo linaukomoo kulingana na ngazi aliyopo mtu.

Na Rukia Chasanika

Wahitimu wa vyuo mbalimbali nchini wameshauriwa kutumia vizuri elimu zao katika kukabiliana na vitendo vya kikatili pamoja na kudumisha maadili mema kwenye jamii.

Wito huo umetolewa na mgeni rasmi katika mahafali ya nane katika chuo cha maendeleo ya jamii KAPS Mbeya, ambaye ni mkuu wa wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Linda Salekwa.

Mkuu wa wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Linda Salekwa(picha na Rukia Chasanika)
Sauti ya mkuu wa wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Linda Salekwa

Mh. Linda amesema wahitimu hao wanatakiwa kuwa chachu ya maendelea  hasa katika kutatua changamoto mbalimbali katika jamii.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Linda Salekwa

Mkuu huyo wa wilaya amesema amesema kuwa serikali ya awamu ya sita inawajali wanachuo wa vyuo vya kati kwa kutoa mikopo hivyo wanatakiwa kuitumia vizuri kusoma kwa bidii.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Linda Salekwa

Kwa upande wake mkuu wa chuo cha maendeleo ya jamii KAPS Mbeya Denis Simbeye amesema mpaka sasa chuo hicho kimetoa maafisa maendeleo ya jamii 3006 ambao wameajiriwa katika ngazi mbalimbali.

Mkuu wa chuo cha maendeleo ya jamii KAPS Mbeya Denis Simbeye(picha na Rukia Chasanika)
Sauti ya mkuu wa chuo cha maendeleo ya jamii KAPS Mbeya Denis Simbeye

Nao baadhi ya wahitimu chuoni hapo wamesema watafanyia kazi mambo yote waliyojifunza ili kuhakikisha jamii inakuwa bora muda wote.

Sauti za baadhi ya wahitimu chuoni