Wakristo wakumbushwa kudumisha amani kuelekea uchaguzi
14 July 2024, 18:23
Kudumisha amani ni jambo linalopaswa kufanya na mtu yeyote kwenye, amani inapotoweka husababisha madhara mbalimbali ilikiwemo vifo ili kuepuka hayo jamii inapaswa kuishi na kuwa sababu ya kutunza Amani, ukiwa ni pamoja na kuwa na mshikamano.
Na Hobokela Lwinga
Katika kuelekea uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa wakristo wamekumbushwa kumtanguliza Mungu kwa kuombea Amani, Upendo na mshikamano katika taifa ili uchaguzi uweze kufanyika kwa Upendo na amani.
Hayo yamesemwa na askofu wa kanisa la Moravian Tanzania jimbo la Kusini magharibi Robert Yondam pangani katika ibada ya uzinduzi wa ofisi za utawala za kanisa la Moravian wilaya ya Chunya ambalo amesema wakristo wanawajibu wakubeba jukumu la kuombea uchaguzi ujao wa viongozi wa serikali .
Aidha mwenyekiti wa wilaya chunya kanisa la moravian Mch.Anyandwile Kajange amewashukuru viongozi wa serikali ya wilaya ya chunya kwa michango mbalimbali kwaajili ya ujenzi wa ofisi za utawala za wilaya ya chunya za kanisa la moravian Tanzania jimbo la kusini magharibi.
Mkuu wa wilaya ya Chunya Alhaji Batenga amewashukuru viongozi wa dini kwa kuunga mkono serikali ya awamu ya sita katika juhudi zinazofanywa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu hassani na kuwaomba viongozi wa Dini kuendelea kudumisha amani.
Hata hivyo Mbunge wa jimbo la Lupa Masache Kasaka amwaomba wakristo kumuombea Rais samia pamoja na kuombea uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa katika uchaguzi ujao.