Baraka FM

Ofisi za utawala kanisa la Moravian wilaya ya Chunya kuzinduliwa

13 July 2024, 10:57

Kanisa la Moravian limekuwa na utaratibu wa mgawanyo wa utawala katika kuwafikisha waumini wake karibu kwenye maeneo mbalimbali hali hiyo inafanya wilaya zake kumiliki ofisi ambazo asilimia kubwa zinajengwa na waumini.

Na Ezekiel Kamanga

Askofu Robert Pangani wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi anatarajia kuzindua ofisi mpya ya Wilaya ya Chunya.

Uzinduzi huo utakaofanyika Julai 14,2024 utaambatana na ibada itayofanyika Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi Ushirika wa Chunya Mjini.

Mwenyekiti wa Wilaya ya Chunya Mchungaji Anyandwile Kajange amesema ujenzi wa ofisi hiyo mpya umetokana na ufinyu wa ofisi ya awali ambayo haikidhi uhitaji uliopo kwa sasa.