Baraka FM

Mke wa mchungaji mstaafu marehemu Amosi Mwasambapa afariki dunia

4 July 2024, 19:28

Duniani tutapata, wote tuko safari na katika safari hiyo hakuna anayejua mwisho wake , yaani mwisho wa uhai wake .

Na Hobokela Lwinga

Katibu Mkuu kanisa la Moravian Jimbo la kusini magharibi Ndugu Israeli Mwakilasa anautangazia umma na waumini wa kanisa la Moravian kuwa Mke wa Mchungaji mstaafu Marehemu mch.Amosi Mwasambapa Sabina Joseph Mwakilembe akafariki dunia.

Mwakilasa amesema Marehemu Sabina Joseph Mwakilembe amefariki Dunia Julai 03 majira ya mchana wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa mkoa wa Mbeya.

“Tumepokea habari za Masikitiko za Msiba wa Mke wa Mchungaji MWASAMBAPA kilichotokea mchana wa Leo. Alifika ibada ya kitulano Ushirika wa nzowe alipoanza kujisikia vibaya alipopelekwa hospital ya rufaa hatimaye akafariki Dunia. Habari nyingine za mipango ya Mazishi tutaendelea kuzipokea na kuwajulisha mara tututakapopokea. Mungu ampumzishe Kwa Amani”.

Kwa upande wake mchungaji wa Ushirika wa nzovwe amesikitishwa na kifo hicho kwani marehemu hakuonesha dalili yoyote ya kuugua na kabla ya kifo chake alishiriki Ibada ya maandalizi ya mkutano wa dinari wa kwaya kuu.

Kabla ya umauti wake Marehemu inadaiwa alishiriki Ibada ya maandalizi ya kwenda kwenda kwenye mkutano wa dinari ya kwaya kuu ambao unatarajiwa kuanza leo Julai 04,2024 katika Ushirika wa mabatini,Marehemu anaumri wa miaka na anatarajiwa kuzikwa jumamosi julai 06,2024.