Baraka FM

Hizi ndizo sababu za kuvunjika kwa ndoa nyingi katika karne ya sasa

3 July 2024, 16:25

Je,unafahamu sababu za kuvunjika kwa ndoa nyingi katika karne ya sasa?Ziko sababu nyingi zinatajwa na inawezekana ukizijua zitakusaidia.

Na Hobokela Lwinga

Mabadiliko ya sayansi na teknolojia yatajwa kuwa sababu kubwa ya ongezeko kubwa la talaka Kwa wanandoa wengi.

Hayo yemesemwa na mwenyekiti wa kanisa la Moravian wilaya ya Mbeya Mch.Osia Mbotwa wakati akizungumza na kituo hiki kuhusiana na ongezeko la migogoro ya ndoa kwenye jamii.

Mwenyekiti wa kanisa la Moravian wilaya ya Mbeya Mch.Osia Mbotwa(picha na Hobokela Lwinga)

Mch mbotwa amesema baadhi ya vijana wengi wamekuwa wakitamani ndoa zinazooneshwa katika mitandao ya kijamii nakutamani jinsi ndoa hizo zinazofanyika kifahari na kuingia katika ndoa kwa matamanio.

Sauti yamwenyekiti wa kanisa la Moravian wilaya ya Mbeya Mch.Osia Mbotwa

Aidha mwenyekiti huyo amesema familia zimekua na mchango mkubwa wa kusababisha ndoa kutokudumu Kwa muda mrefukutokana na malezi hafifu wanayoyatoa.

Sauti ya mwenyekiti wa kanisa la Moravian wilaya ya Mbeya Mch.Osia Mbotwa

Baadhi ya wananchi mkoani hapa wamesema changamoto kubwa ni wanandoa kuingia kwenye ndoa kwa matarajio makubwa ya mahitaji sambamba na mtindo wa maisha.

Sauti za Baadhi ya wananchi