Baraka FM

Mchungaji mstaafu kanisa la Moravian Levant Aaron Sichone afariki dunia

29 June 2024, 06:46

Marehemu mchungaji Levant Aaron Sichone (picha na familia)

Duniani wote tunapita, ndivyo unaweza kusema kwani hakuna anayeijua siku yake ya kutwaliwa hapa duniani ndio maana vitabu vya Dino pamoja viongozi wa kiimani wamekuwa wakisistiza kuishi Maisha ya kumpendeza Mungu wakati wote

Kanisa la Moravian Tanzania jimbo la kusini magharibi linasikitika kutangaza kifo cha mchungaji mstaafu Levant Sichone kilichotokea usiku wa kuamkia Leo 28/06/2024.

Taarifa iliyotolewa na katibu Mkuu wa kanisa Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi Ndugu Israel Mwakilasa inaeleza kuwa marehemu amefariki wakati anapatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa mkoa wa Mbeya.

katibu Mkuu wa kanisa Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi Ndugu Israel Mwakilasa

Aidha katibu Mkuu huyo Amesema utaratibu wa mazishi unaendelea kuratibiwa na kanisa Kwa kushirikiana na familia hivyo utakapokamilika taarifa rasmi itatolewa.

Marehemu mchungaji Levant Aaron Sichone (picha na familia)

“Tumepokea hivi punde taarifa za kifo Cha Mchungaji Mtaafu Mch Levant Sichone kilichotokea usiku wa Kuamkia Leo hapa Hospitali ya Rufaa ambapo alikuwa anatetea Afya yake,Nawapa taarifa za awali Ili kupata taarifa rasmi kutoka Kwa familia utaratibu mzima wa Mazishi. Mungu amuhifadhi mahala pema Amina.”