Baraka FM

Wanawake watakiwa kupeana ujuzi kuyafikia malengo

24 June 2024, 15:47

Baadhi ya wanawake walio shiriki Hafla hiyo(picha na Hobokela Lwinga)

Naibu waziri Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari mhandisi Maryprisca Winfred Mahundi amewataka wanawake wenye malengo ya kujiendeleza kiuchumi kutokuwa wabinafsi katika kupeana ujuzi na maarifa ya mafanikio waliopata na kutembea pamoja bila kuwekeana chuki na husuda kwa mafanikio ya mtu mwingine .

ameyazungumza hayo jana 23/6/2024 jijini Mbeya wakati akizungumza na Umoja wa Wanawake wenye malengo (WOMEN WITH TARGET) katika mkutano mkuu wa kundi hilo ambalo sasa lina mtaji na dhamana ya zaidi ya milioni sita walizojiwekea.

Katika hafla hiyo mhe.Mahundi ametoa rai kwa wanawake kuendelea kupendana bila kuwa na choyo ya ujuzi na uwezo walionao katika kuhakikisha kila moja anakuwa kibiashara.

Naibu waziri Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari mhandisi Maryprisca Mahundi(picha na Hobokela Lwinga)

Katika hatua nyingine Beno Malisa Mkuu wa wilaya ya Mbeya akitoa salamu mbele ya umoja huo amewataka wanawake kuungana mkono katika nafasi za uongozi na kusaidiana kibiashara pasipo kuingia katika mikopo umiza.

Mkuu wa wilaya ya Mbeya mjini Mhe Beno Malisa(picha na Hobokela Lwinga)