Mbeya DC yanufaika na mabilioni ya fedha za Dkt. Rais samia
20 June 2024, 15:21
Shukrani ni sehemu ya kukubali matokeo ya jambo ambalo mtu au watu wanakuwa wamelipata,katika halmashauri ya Mbeya wananchi wameipongeza serikali kupitia ziara ya MNEC Ndele Mwaselela kwa kupeleka maendeleo kwenye maeneo yao.
Na Hobokela Lwinga
Serikali kupitia ilani ya chama cha mapinduzi imeendelea kutoa fedha za maendeleo katika halmashauri ya Mbeya ili kupunguza kero mbalimbali kwa wananchi katika sekta za maji,elimu na miundombinu ya barabara.
Hayo yamebainishwa na mjumbe wa halmashauri kuu taifa wa chama cha mapinduzi mkoa wa Mbeya Ndele Mwaselela wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea matokeo ya ziara yake aliyoifanya kuanzia june 4,2024 katika halmashauri ya Mbeya.
Ndugu Mwaselela amesema katika sekta ya elimu Rais samia ametoa fedha za ujenzi wa shule za kata katika kata ya utengule usongwe na kata nyingine 22 katika halmashauri hiyo.
Aidha katika sekta ya maji amesema serikali imetoa Zaidi ya bilioni 8 kukamilisha mradi wa maji utakaowanufaisha wananchi wa kata ya Isuto na kata jirani sambamba na mrdi wa maji unaoendelea kujengwa mto kiwira unatajwa kuondoa kero ya maji katika mkoa wa Mbeya.
Katika hatua nyingine MNEC huyo amesema serikali imeendelea kuunganisha wananchi kupitia miundombinu ya barabara kwa kujenga barabara inayotoka makete na kuingia halmashauri ya Mbeya.
Sanjari na hayo Mwaselela amesema mji mdogo wa Mbalizi serikali inaujenga kwa mkakati huku akisema mji huo una fursa nyingi za kibiashara kutokana na uwepo wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe.
Baada ya kuhitimishwa kwa ziara hiyo katika halmashauri ya mbeya mnec huyo anatarajia kuanza ziara katika halmashauri za Chunya,Rungwe Kyela Mbarali Na Jiji La Mbeya huku zikiwa zimebeba dhana ya salamu za rais Dkt.Samia na mchakamchaka wa MNEC Mwaselela.