Baraka FM

TARI nchini yawafikia wakuliwa migomba Busokelo,Mbeya

12 June 2024, 12:27

Zao la migomba ni zao la chakula na biashara ,katika nchi ya Tanzania ipo mikoa ambayo imekuwa na uzalishaji mwingi kupitia kilimo hicho ikiwemo mikoa ya Kagera eneo la Bukoba na Mbeya katika halmashauri ya wilaya ya Rungwe na Busokelo.

Na Hobokela Lwinga

Kutokana na zao la ndizi kuwa sehemu ya mazao ya chakula na biashara, Taasisi ya utafiti wa kilimo nchini TARI kituo cha maruku mkoani Kagera kwa kushirikina na TARI UYOLE Mbeya kimetoa elimu ya uzalishaji bora wa zao hilo kwa kupeleka mbegu za migomba ambayo inavumilia ukame na magonjwa ya mnyauko.

Akizungumza wakati wa kutoa elimu katika kata kisegese halmashauri ya wilaya ya Busokelo afisa msaidizi kutoka Taasisi ya utafiti wa kilimo TARI kituo cha Uyole Mbeya Joseph Mdede amesema wakulima wanapaswa kutumia mbegu bora ili kupata mazao yenye ubora.

Afisa msaidizi kutoka Taasisi ya utafiti wa kilimo TARI kituo cha Uyole Mbeya Joseph Mdede (picha na Hobokela Lwinga)

Kwa upande wake afisa utafiti kutoka katika kituo cha utafiti cha Maruku mkoani Kagera Joseph Kimisha amesema zaidi ya wananchi 50 wa awali watanufaika na utafiti wa mbegu hizo na hao ndio watakuwa shamba darasa kwa wakulima wengine.

Baadhi ya wakulima wakishiri kupata elimu ya upandaji bora wa zao la mgomba (picha na Hobokela Lwinga)

Hata hivyo wakulima wa ndizi walionufaika na elimu hiyo wamesema elimu hiyo itakuwa kichocheo cha kupata tija ya kilimo cha ndizi kwani awali walikuwa wanalima kwa mazoea.

Afisa msaidizi kutoka Taasisi ya utafiti wa kilimo TARI kituo cha Uyole Mbeya Joseph Mdede akitoa elimu ya upandaji bora wa migomba(Picha na Hobokela Lwinga)