Askofu Nguvumali wa Moravian,atangaza kustaafu September 2025
12 June 2024, 11:56
Kanisa la Moravian kupitia katiba za majimbo yake limekuwa utaratibu wa ukomo wa uongozi unaoendana na umri,hali hiyo inaleta mabadiliko ya Kiongozi kwani inatoa fursa ya kufanya uchaguzi upya wenye demokrasia.
Na Hobokela Lwinga
Askofu Kiongozi kanisa la Moravian Tanzania na askofu Jimbo la Rukwa Mhashamu Conrad sikombe Nguvumali ameomba ushirikiano kwa Askofu mpya wa kkkt dayosisi ya ziwa Tanganyika Imani Chibona katika kumtangaza Kristo katika mkoa wa Rukwa.
Ombi hilo amelitoa wakati akiwasilisha salamu za jumuiya ya kikristo Tanzania CCT katika ibada maalum ya kuwekwa wakfu na kuingizwa kazini kwa Mkuu wa Dayosisi ya ziwa Tanganyika Askofu Imani Chibona na msaidizi wake Zebedayo Mbilinyi iliyofanyika katika kanisa Kuu la KKKT usharika wa Sumbawanga mjini.
Askofu Nguvumali Amesema jukumu la viongozi hao wanaoingizwa kazini wanapaswa kuenzi neema ya unyenyekevu ili waweze kuitenda kazi ya Mungu katika utukufu wa Mungu aliouweka ndani yao.
Katika ibada hiyo askofu Nguvumali ametangaza rasmi kustaafu mwezi September 2025 na ameomba aombewe ili astafu vyema.