Baraka FM

Askofu Pangani:lindeni amani ya kanisa na Taifa

11 June 2024, 11:26

Kila mwananchi anawajibu wa kuendelea kulinda taifa lake kwa kulinda amani, kuanzia katika ngazi ya familia

Na Hobokela Lwinga

Askofu wa kanisa la Moraviani Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi Mhashamu Robert Pangani amewataka wakristo wote kuilinda Amani ya kanisa na taifa.

Hayo ameyasema Leo katika ibada ya pili baada ya utatu katika kanisan la Moravian Tanzania ushirika wa Jacaranda ambapo ndipo yalipo Makao makuu ya Kanisa hilo.

Amesema msingi wa mkristo ni kuwa kielelezo cha kuzalisha amani kama Kristo alivyoliachia kanisa amani.

Katika hatua nyingine Askofu Pangani amesema kuwa anaetakiwa kuabudiwa ni Mungu na sio mwanadamu kwani Mungu ndie muumba wa haya yote yaliyopo sasa.

Ikumbukwe kuwa ibada ya maalumu ya kumsimika Askofu Pangan ilifanyika Tarehe 2 mwezi wa 6 mwaka 2024 katika viwanja vya Chuo Kikuu Teofilo Kisanji (TEKU) cha kanisa la Moravian oravian Tanzania.