Baraka FM

Wazazi zingatieni malezi bora ya watoto

4 June 2024, 14:52

Inspetar Dastani Nikata(kushoto)na kulia ni inspetar Christopher Zambi wakitoa elimu katika studio za radio Baraka(picha na ivillah Mgala)

Malezi bora ya mtoto ndiyo yanategemea zaidi uwepo wa maadili bora kwenye jamii na endapo jamii itakosa maadili bora kwa watoto basi jamii hiyo itakuwa na kizazi ambacho kitakuwa hakina maadili mazuri.

Ivillah Mgala

Wazazi wametakiwa kuwalea watoto katika maadili mema ili kupunguza vitendo vya kiharifu katika jamii zao.

Hayo yamesemwa na inspetar Christopher Zambi wakati akizungumza na kituo hiki juu ya umuhimu wa vikundi shirikishi katika jamii.

Inspetar Zambi amesema kama wazazi watasimama katika nafasi zao za malezi bora ya watoto wao wahalifu watapungua katika jamii.

Inspetar Christopher Zambi akieleza umuhimu wa malezi bora kwa watoto(picha na Ivillah Mgala)

kwa upande wake Inspetar Dastani Nikata ameviomba vikundi vya ulinzi shirikishi kufwata kanuni za vikundi hivyo ili kutovunja sheria.