Hatimaye mch.Robart Pangani awa askofu kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi
3 June 2024, 11:53
Kanisa la Moravian jimbo la kusini magharibi wakiongozwa na maaskofu wa kanisa hilo Tanzania wameshiriki Ibada ya kumuweka wakfu Askofu wa kanisa la Moravian Tanzania jimbo la kusini magharibi Mchungaji Robert Pangani.
Na Ezra Mwilwa
Wachungaji na wakristo wa kanisa la Moravian Tanzania jimbo la kisini Magharibi wametakiwa kumuuombea na kuonyesha ushirikiano.
Hayo yamesemwa na Askofu wa kanisa la Moravian jimbo la Magaribi Tabora Askofu Ezekiel Yona wakati akihubiri katika ibada ya kumuweka wakfu Askofu huyo mteule katika viwanja vya chuo kikuu TEKU jijini Mbeya.
Askofu Ezekiel ameongeza kuwa katika kuitenda kazi ya Uaskofu aepuke kutengeneza matabaka kwa viongozi wa kanisa ngazi tofauti tofauti ndani ya jimbo.
Mgeni Rasmi katika Ibada hiyo Mhe.Dkt. Dotto Biteko ambaye ni naibu waziri Mkuu na waziri wa Nishati akimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amesema kama wakristo tuendelee kumuombea na kutii mamlaka ya iliyowekwa na Mungu sambamba na kuhamasisha amani na upendo.
Nae Mbunge wa jimbo la mbeya mjini, spika wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa mabunge Duniani Dkt. Tulia Akson amesema yeye kama Mbunge na wananchi ana Imani kuwa askofu Pangani atatuongoza vema katika kuilinda amani na Utulivu ndani ya kanisa.
Aidha Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera amesema anamshukuru Rais Samia Suluhu kwakuziunganisha taasisi za Dini na kumwomba naibu waziri Mkuu kusaidia kutatua mgogoro wa kiwanja cha kanisa la Moravian Tanzania kilichopo jijini Dodoma.
Askofu Robert Pangani akitoa shukrani amesema yeye kama Askofu anadeni kubwa la kulitumikia kanisa na serikali kwa na ameipongeza serikali kwa kuonyesha ushirikiano kwa viongozi wa Dini.