Baraka FM

Mbeya Dc kinara uzalishaji zao la Pareto nchini

1 June 2024, 07:15

Nyuma ni wakulima wa zao la Pareto wakiwa na afisa pareto kutoka kampuni ya ununuzi wa Pareto Tanzania PCT ndugu Musa Malubalo (aliyevaa kofia).

Pareto ni zao la biashara linalotumika kutengenezea viuatilifu mbalimbali vya kuua wadudu wanao tambaa na kuruka.

Na Hobokela Lwinga

Mkuu wa wilaya ya Mbeya mhe.Beno Malisa amesema mnunuzi yeyote ambaye atakiuka miongozo katika katika kununua zao la pareto atachukuliwa sheria ikiwa ni pamoja na mawakala wa makampuni husika.

Mkuu huyo ameyasema hayo katika Kikao kazi cha wadau wa zao la Pareto kuhusu umhimu wa kufuata sheria na kanuni zao la pareto kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa GR comfort kabwe jijini Mbeya.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Mbeya mhe.Beno Malisa

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya ameyataka makampuni yote ya ununuzi wa Pareto katika halmashauri ya Mbeya kulipa kodi na atakaye kiuka mkono wa sheria utachukua mkondo wake.

Mkuu wa wilaya ya Mbeya mhe.Beno Malisa(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Mbeya mhe.Beno Malisa

Awali akizungumza mkurugenzi mkuu bodi ya Pareto nchini Lucas Kiayo amesema halmashauri ya Mbeya ndiye kinara wa uzalishaji wa zao la pareto ambapo ni asilimia 85 pareto inazalishwa katika halmashauri hiyo.

Mkurugenzi mkuu bodi ya Pareto nchini Lucas Kiayo(picha na Hobokela Lwinga)

Afisa kilimo na mifugo halmashauri ya Mbeya Gidion Mapunda amesema kwa sasa wanunuzi wote wanapaswa kufuata mashariti ya ununuzi ikiwa ni pamoja na kununua kwenye vituo mahususi sambamba na kutokununua pareto mbichi.

Afisa kilimo na mifugo halmashauri ya Mbeya Gidion Mapunda(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya afisa kilimo na mifugo halmashauri ya Mbeya Gidion Mapunda

Baadhi ya wadau wa kilimo cha pareto na wanunuzi wa zao hilo Gerald Joseph kutoka PCT na Musa mnasi SHANATEC LIMITED wameiomba serikali kuingilia kati kilimo cha Pareto ili kiendelee kuzalishwa kwa ubora.

Baadhi ya washiriki wa kikao kazi kutoka kampuni ya ununuzi wa zao la Pareto PCT (Picha na Hobokela Lwinga)
Sauti zaBaadhi ya wadau wa kilimo cha pareto na wanunuzi wa zao hilo Gerald Joseph kutoka PCT na Musa mnasi SHANATEC LIMITED