Baraka FM

MNEC Mwaselela apeleka kicheko kwa vijana Mbeya

27 May 2024, 20:20

Wanafunzi wa vyuo vikuu na kati mkoa wa Mbeya waliopo ndani ya UVCCM wakiwa katika mahafari (picha na Lukia Chasanika)

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama Cha mapinduzi CCM Taifa Mnec, Ndele Mwaselela amesema kuwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan anajivunia vijana kuwa ndio nguvu kazi ya Taifa.

Na Lukia Chasanika

Mnec Mwaselela ameyasema hayo akiwa mgeni rasmi katika mahafari ya seneti ya vyuo vya kati na vyuo vikuu chama cha mapinduzi mkoa wa Mbeya iliyofanyika katika ukumbi wa Tughimbe mkoani hapa.

Mwaselela amesema kuwa Rais Dkt.Samia anatenda haki kwa kila mmoja hivyo vijana wasiogope kugombea katika nafasi mbalimbali za uongozi na waendelee kuhuburi umoja na mshikamano bila kujali itikadi zao za vyama na dini zao.

Sauti ya mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa Ndele Mwaselela

Kwa upande wao baadhi ya wahitimu katika hafla hiyo wamemshukuru Rais Samia Suluhu na MNEC kwa moyo huo wa kipekee wa kukubali kushuka kwa watu wa chini na kuonyesha upendo wa aina yake ikiwa ni pamoja na kuongeza bumu kwa wanafunzi wa vyuo na vyuo vikuu hadi kufikia shilingi elfu kumi.

Baadhi ya wahitimu wakikabidhiwa vyeti na MNEC Ndele Mwaselela(picha na Lukia Chasanika
Sauti za baadhi ya wahitimu wakitoa shukrani zao

Katika risala yao wahitimu wamesema wanakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na mradi pamoja na vifaa vya kuendeshea shughuli mbalimbali za umoja wao.

Akijibu risala yao mhe.Mwaselela amewapatia kiasi Cha shilingi milioni mbili za mtaji pamoja na vifaa vya kutunzia kumbukumbu zao ikiwemo komputa pamoja na printer.

Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi mkoa wa Mbeya mhesimiwa Ndele Mwaselela (kushoto) akikabidhi Computa(picha na Lukia Chasanika)
Sauti ya MNEC Ndele Mwaselela akikabidhi Compyuta