Baraka FM

NEMC kuwafikia wachimbaji madini zaidi ya 300 Mbeya, Songwe

21 May 2024, 22:40

Baadhi ya Wachimbaji walioshiriki mafunzo(picha na Kelvin Lameck).

Sekta ya madini ni sekta nyeti katika kuliingizia taifa pato,katokana na hali hiyo serikali imeendelea kuwatengenezea mazingira rafiki wachimbaji sambamba na kutoa elimu ya mara mara ili kujiepusha na madhara wanayoweza kuyapata kutokana na kazi ya uchimbaji.

Na Kelvin Lameck

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC kwa kushirikiana na ofisi ya mkemia mkuu wa serikali nchini limetoa mafunzo ya udhibiti wa kemikali ya zebaki kwa wachimbaji wadogo wa madini katika mji wa Makongorosi wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Mhandisi kutoka baraza la taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira Boniface Kyaruzi amesema baraza hilo litaendelea kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo ili kuwaongezea ueledi katika kulinda afya zao na kutunza mazingira.

Sauti ya mhandisi kutoka baraza la taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira Boniface Kyaruzi

Mhandisi Kyaruzi ameongeza kuwa kutokana na athari za matumizi holela ya Zebaki wamedhamiria kuwafikia zaidi ya wachimbaji mia tatu kwa Chunya na Songwe ili kuwapa elimu hiyo yenye manufaa kwa afya zao.

Mhandisi kutoka baraza la taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira Boniface Kyaruzi(picha na Kelvin Lameck)
Sauti ya mhandisi kutoka baraza la taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira Boniface Kyaruzi

Naye meneja wa usajili maabara sayansi jinai na vina saba kutoka ofisi ya mkemia mkuu wa serikakali Joyce Njisya amesema lengo la mafunzo hayo ni kutoa elimu kwa wachimbaji ili waweze kutumia njia sahihi za matumizi ya kemikali hiyo.

Sauti ya meneja wa usajili maabara sayansi jinai na vina saba kutoka ofisi ya mkemia mkuu wa serikakali Joyce Njisya

Akizungumzia madhara ya kiafya yatokanayo na matumizi mabaya ya Zebaki Mkemia Mwandamizi kutoka mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali Zabibu Rashid amesema ni pamoja na kuharibika kwa mimba, kuathirika viungo vya ndani kama moyo na figo, kutembea na ukakamavu,kuathiri mfumo wa kusikia na kuona.

Kwa upande wao baadhi ya Wachimbaji walioshiriki mafunzo hayo wameishukuru serikali kupitia NEMC kwa kuwapa elimu juu ya madhara ya kemikali ya Zebaki na kwamba watakuwa mabalozi wazuri kwenye utunzaji wa mazingira.

Sauti zabbaadhi ya Wachimbaji walioshiriki mafunzo